John 3:22-26

22 aBaada ya haya, Isa na wanafunzi wake walikwenda katika nchi ya Uyahudi, nao wakakaa huko kwa muda na kubatiza. 23 bYahya naye alikuwa akibatiza huko Ainoni karibu na Salimu kwa sababu huko kulikuwa na maji tele. Watu wazima wakamjia huko ili kubatizwa. 24 c(Hii ilikuwa kabla Yahya hajatiwa gerezani). 25 dMashindano yakazuka kati ya baadhi ya wanafunzi wa Yahya na Myahudi mmoja kuhusu suala la desturi ya kunawa kwa utakaso. 26 eWakamwendea Yahya wakamwambia, “Rabi, yule mtu aliyekuwa pamoja nawe ng’ambo ya Mto Yordani, yule uliyeshuhudia habari zake, sasa anabatiza na kila mtu anamwendea!”

Copyright information for SwhKC